Viongozi na wadau wanaosimamia sekta ya misitu na mazao yake mkoani Morogoro wametakiwa kuwa na ushirikiano wa karibu katika kutekeleza majukumu yao hususani kwenye kukabiliana na wasafilishaji haramu wa mazao ya misitu .
Mwakilishi wa mkurugenzi mkazi wa Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori (WWF) Tanzania, meneja uhifadhi kutoka WWF Dk Laurence Mbwambo alitoa ushauri huo wakati wa hafla ya kuutambulisha mradi wa matumizi sahihi ya nishati safi na salama.
Dk Mmbwambo alisema ili kukabiliana na wasafilishaji haramu wa mazao ya misitu lazima kuwepo na ushirikiano kutoka Jeshi la Polisi hususani askari wa usalama barabarani(trafiki)na wataalamu wa Wakala wa Misitu Tanzania(TFS).
Aidha alisema kuwa Kwa sasa wasafilishaji haramu wa mazao ya misitu ikiwemo mkaa wameshamili hasa wale wanaobeba mkaa na pikipiki wamekuwa pia wakikwepa kulipa ushuru na kuikosesha serikali mapato, hivyo basi ni muhimu hawa watu wafanyiwe kazi ili kutokomeza shughuli hiyo haramu.
“Kusafilisha mkaa kwa pikipiki ni kinyume na Sheria, hivyo basi kinachotakiwa ni elimu Kwa wananchi lakini pia na kuisimamia Sheria Ili watu waweze kufanya shughuli zao Kwa kufuata Sheria na kanuni za serikali,”alisema Dk Mbwambo.
Naye kaimu katibu tawala msaidizi upande wa rasilimali watu mkoa wa Morogoro Herman Tesha alisema mradi huu umekuja wakati sahihi ambapo kumekuwepo na uharibifu mkubwa wa mazingira hususani kukati miti ya mkaa na Kuni Kwa ajili ya kupata nishati Kwa matumizi ya nyumbani.
Aidha Tesha alisema kuwa tatizo la ukataji miti hovyo ni kubwa sana hivyo basi wadau wa mazingira waendelee kuiunga serikali mkono Kwa kutunza mazingira na wananchi waunge mkono serikali Katika kutumia nishati safi na salama Ili kupunguza tatizo hilo kama si kumaliza kabisa.
Kwa upande wake mratibu wa mradi wa kujengewa uwezo taasisi zinazosimamia masuala ya misitu Tanzania Savinus Kessy alisema kuwa lengo la mradi huo ni kutunza mazingira na kuzuia kabisa masuala ya ukataji miti hovyo na kuharibu mazingira.