Viongozi Wa Chuo Cha Taifa Cha Ulinzi (NDC) Wamepongeza Uwekezaji Wa Viwanda Mbali Mbali Mkoani Manyara Unaolenga Kukuza Ajira Na Kuchangia Maendeleo Ya Taifa Kupitia Ulipaji Kodi Wa Hiyari Na Kuwataka Wawekezaji Kupanua Wigo wa uwekezaji ili Kuongeza manufaa zaidi kwa nchi.
Wakizungumza Mara Baada Ya Kutembelea viwanda mbalimbali mkoani manyara Viwanda ikiwemo Kiwanda Cha Mati Super Brand Limited, Viongozi Wa Chuo Hicho Pamoja Na Wanafunzi Kutoka Mataifa Mbali Mbali barani Afrika Wameeleza Kufurahishwa Na Kasi Ya Uwekezaji Wa Viwanda Unaotokana Na Sera Nzuri Za Nchi Ya Tanzania
Ziara Ya Hiyo Ni Ya Mafunzo ambapo Maafisa Wa Chuo Hicho Wamejifunza Mambo Mbali Mbali ikiwemo uzalishaji wa bidhaa za viwandani na usalama wa chakula.
Chuo cha Taifa cha Ulinzi kilianzishwa mwaka 2011, NDC ndicho chuo kikuu cha mafunzo ya kimkakati na taasisi kuu ya mafunzo ya Wizara ya Ulinzi.