Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amewaomba viongozi wa dini kukemea baadhi ya maneno yanayotamkwa na wanasiasa badala ya kukaa kimya.
Ametoa ombi akiongea na viongozi wa dini Visiwani Zanzibar, kuhusuiana na suala la amani, katika kipindi chote cha uchaguzi ambapo amesema viongozi wa dini ni moja ya wadau wa amani nchini.
“Niwaombe sana kwa sababu mnasikia baadhi ya maneno yanayotamkwa na baadhi ya wanasiasa lakini mmekaa kimya hamsemi, mmekaa kimya hamkosoi, mmekaa kimya mekuwa woga niwaombe sana ni muda sasa kuona kuna jambo linaenda ndivyo sivyo tulikemee”IGP Sirro.
“Padri ukishajiingiza kwenye uhalifu mimi ntakushughulikia kama uhalifu mwingine, Padri ukishakuwa mbakaji ntakugonga kama mbakaji mwingine, Shehe/Padri ukijiingiza kwenye ugaidi ntakushughulikia kama gaidi hiyo kwasababua heshima ina ukubwa zaidi kuliko mtu binafsi” IGP Sirro.
MAPOKEZI YA KUNAMBI JIMBONI MOROGORO, ACHUKUA FOMU