Viongozi wa dini watakiwa kuwa mstari wa mbele kukemea vitendo viovu katika Jamii badala ya kuiachia Serikali pekee yake ili kulinda Maadili ya vijana na watoto.
Wito huo umetolewa na Mwalimu Augustine Tengwa wakati akizungunza na wanahabari Mkoani Morogoro kuhusu mwenendo wa Mtindo wa maisha wa vijana kubadilika siku hadi siku kwa kujihusisha na mambo mabaya kama yakiwemo mapenzi ya Jinsia Moja ,kinyume na maumbile pamoja na wanaume kusuka nywele jambo ambalo linahatarisha vijana wengi na kuiga kwa lengo la kupata fedha.
Anasema siku za hivi karibuni ametembelea mikoa mbalimbali ikiwemo Lindi,Ruvuma,Njombe,Mtwara na Iringa na kushuhudia vijana wakijingiza kwenye mambo yasiyofaa ikiwemo utumiaji Dawa za Kulevya pamoja na biashara haramu ya binadamu kwa kisingizio cha ugumu wa maisha .
“Unakuta Kijana wa kiume amesuka.nywele ,amevaa hereni hana tofauti na mke wake haya mambo tusipokemea Sasa yanzidi kukua tutakua na kizazi Cha hivyo badae”
Naye msaidizi wa kiongozi wa huduma ya maombi kitaifa Alpha Kihamba amesema mpango wao ni kuzunguka nchi nzima kwenye nyumba za ibada ,vijiwe vya bodaboda na maeneo ya mikusanyiko kuzungumza na Jamii kwa kushirikisha na serikali na watu maarufu.
Anasema kuna haja viongozi wa dini kuungana kwa pamoja katika vita hii kubwa ya matumizi dawa za kulevya, biashara haramu ya binadamu pamoja na vitendo vya uhalifu Kwani wananguvu kubwa ya kuzungumza na Jamii na kueleweka Kwa haraka zaidi.
Kwa upande wake Nassoro Boazi amesema kwa sasa nguvu Kubwa inahitajika ili kunusuru kizazi kijacho ambapo wazazi ,Serikali ,wadau na viongozi wa dini wanatakiwa kuwa kitu kimoja