Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kupitia Kamishna wake wa Maadili, Jaji Mstaafu Harold Nsekela imesema kuanzia sasa Viongozi wa Umma wataanza kujaza fomu ya tamko kuhusu rasirimali na madeni katika Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa njia ya mtandao.
Amesema njia hiyo sasa itasaidia kupunguza usumbufu, Upotevu wa nyaraka na uchelewaji wa kufika kwa tamko la kiongozi kutoka maeneo mbalimbali nchini.