Viongozi wa ngazi za vijiji,kata na wilaya za Korogwe na handenin zaidi ya mia na hamsini wamepewa Elimu juu ya Utunzaji wa mazingira na usimamizi wa vyanzo vya maji.
Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo Mratibu wa mradi wa sauti Youth World Vision Shukran Dickson amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kuangalia namna bora ya kutatua changamoto ya uharibifu wa mazingira.
“Unajua hapa Korogwe tumekuwa na changamoto kubwa ya uvunaji wa mazao ya misitu hivyo kwasasa tunapitishana kwenye kanuni na taratibu zilizowekwa ili kufahamu sheria mbalimbali za uvunaji wa mazao ya misitu pamoja na utunzani wa vyanzo vya maji ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi”Alisema Shukran
Aidha shukran alitoa wito kwa Viongozi na kuwataka kuzisimamia sheria zilizo weka na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kusimamia Mazingira na kutunza vyanzo vya maji ili hayo mazingira yasi haribike kwani tunapo haribu mazingira tuna haribu maisha ya kizazi cha sasa na baadaye kwani mazingira ni uhai.
Hata hivyo amesema kuwa mradi huo wa sauti vijana unao fanyakazi katika Wilaya ya Korogwe na handeni una fadhili na shirika la umoja wa Ulaya EU kwabajeti ya 1.6 bilion kwa miaka mitatu.
Kwaupande wake Bob matunda ambaye ni muhifadhi msaidizi katika msitu wa AMANI ametoa wito kwa wenye viti wa vijiji kufata taratibu za utunzaji wa mazingira pamoja na vyanzo vya maji kwa kuweka Sheria ndogo ndogo zitakazo wawezesha wananchi kuto kuvuna misitu wala kuharibu vyanzo vya Maji.
Joyces Malekela Mhandisi wa maji RUWASA Wilaya ya Korogwe alisema kuwa kutokana na Uharibifu mkubwa wa Mazingira umepelekea vyanzo vingi vya maji kukauka na hivyo kuathiri upatikanaji wa maji kwa wananchi na hivyo ametoa rai kwa wananchi kutunza mazingira kwa kupanda miti kwenye vyanzo vya Maji .