Mtu mmoja ambaye alithibitishwa kuwa na maambukizi ya Hanta Virus amefariki dunia akiwa kwenye basi katika Jimbo ya Yunnan. Abiria wengine 32 waliokuwa kwenye basi hilo wamefanyiwa vipimo kuona kama wameathirika.
Kifo hicho kimekuwa gumzo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kutokana na wengi kukifananisha na Corona Virus, ambayo pia ilianzia China.
Imeelezwa kuwa, Hanta Virus husambazwa na Panya wenye Virusi hivyo na ni vigumu kwa watu kuambukizana.
Kwa mujibu wa Kituo cha kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Marekani (CDC), mtu anaweza kuambukizwa pale anaposhika macho, pua au mdomo wake baada ya kushika haja, mkojo au mate ya Panya.