Uholanzi na Ubelgiji zimepiga marufuku ndege kutoka Uingereza huku Ujerumani pia ikitafakari kuchukua hatua kama hiyo kufuatia kugunduliwa kwa aina mpya ya kirusi cha corona kinachoenea kwa kasi zaidi.
Ujerumani inatafakari kupiga marufuku ndege za abiria kutoka Uingereza na Afrika Kusini ili kuzia kuenea kwa aina mpya ya virusi vya corona ambavyo vinaenea kwa kasi sana na ambavyo vimethibitishwa katika Mataifa hayo mawili.
Hatua hiyo itafuata mfano wa Uholanzi, ambayo imepiga marufuku ndege zote za abiria kutoka Uingereza kuanzia Jumapili.
Kulingana na duru hiyo, Serikali ya Ujerumani inatafakari marufuku hiyo kama njia muhimu ya mbadala kuepusha maambukizi zaidi.
Msemaji wa wizara ya afya Ujerumani, amesema serikali inafuatilia kwa karibu hali ilivyo Uingereza na inafanya kazi katika shinikizo kubwa kutathmini tarifa mpya pamoja na data kuhusu aina hiyo mpya ya kirusi.