Mara baada ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kuruhusu visiwa vidogo vidogo kukodishwa mwaka 2021 ambapo kati ya visiwa vidogo17 kwenye 20 vilitangzwa na kupewa wawekezaji kwa kuekeza na thamani ya mitaji ilioekezwa kwenye miradi hiyo ni Dola za kimarekani Milioni 384 ,zaid ya Dola za Kimarekani Milioni 20.5 zimekusanywa kama ada ya visiwa hivyo.
Katibu Mkuu Uchumi na Uwekezaji Afisi ya Rais kazi Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Khamis Mwalim amesema Zaid ya ajira 7000 zinatarajiwa Baada ya ufunguzi wa mradi huo kwenye Kisiwa cha Bawe kilichopo Mkoa wa Mjini Unguja kilichopewa wawekezaji wa kigeni wa Nchini Italy na kuwekeza mtaji wa Dola za Kimarekani Milioni 37
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa maara ya kwanza anatarajiwa kuzindua mradi wa Hoteli Mwezi Juni mwaka huu ikiwa ni kisiwa cha kwanza kati 17 vilivyokodishwa kwa serikali ya Zanzibar kwa uwekezaji