Afisa mmoja ambaye alikuwa miongoni mwa Maafisa wanaosimamia mazungumzo ya kumaliza vita kati ya Ukraine na Urusi, Denis Kireev ameuawa kwa kupigwa risasi, Denis ambaye alikuwa ni Jasusi (Spy) aliyeajiriwa kwenye kitengo cha Intelejensia ya Wizara ya Ulinzi ya Ukraine ameuawa pamoja na Maafisa wenzake wawili.
Wizara ya Ulinzi ya Ukraine imesema Maafisa hao wameuawa wakati wakitekeleza majukumu yao ya kikazi na wamewaita Mashujaa lakini zipo taarifa ambazo zinadai Denis na wenzake wameuawa na Jeshi la Ukraine baada ya kubaini kuwa Maafisa hao wanatumika na Urusi kuichunguza Ukraine.
Ayo TV & Millardayo.com imekuandalia taarifak kamili unaweza ukabonyeza play kufahamu zaidi
RAIS WA UKRAINE AMPIGIA SIMU BIDEN ‘WAJADILI VIKWAZO DHIDI YA URUSI’