Vita vya Gaza vimegharimu uchumi wa Israel zaidi ya dola bilioni 67.3, wanauchumi wa Israel walisema.
“Vita tayari vimegharimu uchumi wa Israel zaidi ya bilioni 250 (dola bilioni 67.3), na taasisi ya ulinzi inataka ongezeko la kila mwaka la angalau NIS bilioni 20 (dola bilioni 5.39),” Rakefet Russak-Aminoach, Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Benki ya Israel. Leumi, aliiambia Idhaa ya 12 ya Israel.
“Upungufu ni mkubwa zaidi. Tuna wakimbizi, waliojeruhiwa, na mahitaji mengi ya kiuchumi ambayo hata hayahesabiwi katika gharama ya vita,” aliongeza.
Mgogoro wa kiuchumi unaendelea kuiathiri Israel, huku ikiwa imepita zaidi ya miezi 10 tangu utawala huo katili ulipoanzisha mauaji ya kimbari katika ukanda wa Gaza, na hadi sasa umeawa shahidi Wapalestina zaidi ya 40,000 ukisaidiwa na nchi za Magharibi husuan Marekani, na nchi za Ulaya kama Uingereza na Ujerumani.
Vyombo vya habari vya Israel pia vinakiri kwamba, vita vya Gaza ndio vita vya “umwagaji damu zaidi” vya karne hii.