Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dorothy Gwajima amempongeza Diwani wa Viti Maalum Kibaha Mjini, Lydia Mgaya kwa kujenga Kituo cha Kulelea Watoto Yatima.
Waziri Gwajima ametoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika ujumbe ufuatao.
“Mungu jalia tupate vinara wenye nafasi kama hawa nchi nzima wenye moyo tuwape semina ya kutosha, vita hii inakuwa tayari ushindi mikononi. Mhe unastahili pongezi wewe Shujaa”.
Itakumbukwa kuwa Lydia ni miongoni mwa diwani anayetajwa kuwa kinara wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ambapo ameiambia millardayo.com kuwa;
“Hii vita ya ukatili sio ya mmoja na inaendana sambamba na mabadiliko ya mifumo mbalimbali, hatuwezi kupinga ukatili kwa mitandao bila utekelezaji mie nimejenga Kituo cha Yatima ambacho awali kilikuwa hakifai hii yote ni kuonyesha jinsi gani navyohakisha tunatokomeza ukatili. Namshukuru Waziri Gwajima kwa kuona jitihada hizi,”.