Meli Iliyobeba Viuatilifu aina ya Salfa zaidi Ya Tani elfu Tano imewasili katika Bandari
Ya Mtwara mapema asubuhi ya leo ambapo viuatilifu hivyo Vitagaiwa bure Kwa wakulima wa Zao la korosho.
Akiongea na Ayo tv Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho amesema “Viuatilifu Hivyo aina ya Salfa vinasaidia kuikinga Mikorosho Isishambuliwe na ugonjwa wa Ubwiriunga hivyo Itaongeza uzalishaji zaidi”
Pia Kaimu Meneja wa Bandari ya Mtwara Norbert Kalembwe amesema “kuwasili Kwa meli hiyo ni matokeo chanya ya serikali ya kufanya upanuzi wa Bandari na kwamba tayari viuatilifu hivyo vimenza kushushwa tayari kupelekwa Kwa wakulima”