Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara umesema hadi sasa, kuna jumla ya Viwanda na Taasisi 12 ambazo zinatengeneza vifaa tiba kama Barakoa, Vitakasa mikono na mavazi maalum kwa watoa huduma za afya nchini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa akisoma Bajeti ya Wizara yake Bungeni leo May 5, 2020.
Aidha, Viwanda vidogo 55 vya nguo na mavazi pia vimeunga mkono kwa kuanza kutengeneza barakoa kwa kutumia malighafi ya kitambaa.
Vivyo hivyo, viwanda vya kutengeneza vitakasa mikono vilivyosajiliwa hadi sasa vimefikia 40.