Baada ya kuripotiwa kuwa Serikali ya Tanzania imejiondoa kwenye mchakato wa kuwa na Viza moja itakayotumika kwa masuala ya utalii katika nchi zote za Afrika Mashariki, Wizara ya Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imetoa tamko kuhusiana na taarifa hizo.
Serikali imesema suala la uanzishwaji wa Viza ya pamoja ya Afrika Mashariki bado liko kwenye majadiliano ya nchi wanachama kupitia vikao vya Sekta ya Utalii na Wanyamapori, na katika kufanikisha kusudio hilo Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Maliasili na Usimamizi wa Wanyamapori uliofanyika November 1, 2008 liliunda kikosi kazi kwaajili ya kufanya utafiti kwa lengo la kubainisha mahitaji na utayari wa nchi wanachama.
Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeeleza kuwa katika vikao vilivyofanyika mwaka 2010 kulikua na masuala muhimu ambayo yanatakiwa kuzingatiwa kabla ya kuanzisha kwa Viza ya pamoja ya Utalii. Millardayo.com inakuletea mambo 6 yaliyobainishwa kwenye mkutano huo.
- Kurazinisha (Harmonization) sheria za Viza za Nchi Wanachama.
- Idara ya Uhamiaji kuanzisha Mfumo wa kudhibiti Usalama.
- Utoaji wa Viza kuwa wa Kielektroniki.
- Kuwepo kwa mfumo wa ukusanyaji na ugawanyaji wa mapato pamoja na namna ya kuyalipa.
- Kuwepo kwa maafisa uhamiaji katika ofisi za ubalozi.
- Kujenga uwezo wa watumishi kwenye suala la mfumo wa kielektroniki wa utoaji Viza ya pamoja.
Kufuatia matokeo ya utafiti huo, mkutano wa 5 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori uliofanyika Julai 2013 jijini Bujumbura Burundi uliagiza kuundwa kwa kamati itakayojumuisha wataalamu kutoka Taasisi za Uhamiaji, Utalii, Fedha, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Tehama, Usalama na Sheria katika nchi wanachama ili kuandaa mpango kazi na kushughulikia mambo yote ya uanzushwaji wa Viza hiyo.
Hata hivyo kabla ya utekelezaji wa maagizo hayo, nchi za Uganda, Kenya na Rwanda zilianzisha Viza ya pamoja ya Utalii kwenye nchi zao ikiwa ni nje ya vikao vya jumuiya.
Taarifa ya Benard Haule ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Biashara Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeeleza kuhusu tamko hili.
Unaweza kutazama hapa.
ULIPITWA NA UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA LEO OCTOBER 19, 2016? TAYARI NIMEYAWEKA HAPA