Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ameliagiza Jeshi la Polisi kushirikiana na Wakala wa Barabara (TANROADS) pamoja na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kufanya ukaguzi katika maeneo yote nchini yenye vizuizi na vituo vya ukaguzi, kuangalia kama vimewekwa kwa kuzingatia sheria na tahadhari za usalama kwa watumiaji wengine wa barabara na kama vipo katika maeneo hatarishi viondolewe.
Bashungwa ameeleza kuwa taarifa za ajali mbalimbali zimeonesha dosari kwa baadhi ya vizuizi na vituo vya ukaguzi barabarani, kutozingatia matumizi sahihi ya barabara na hivyo kusababisha ajali.
Amelisisitiza Jeshi la Polisi kushirikiana na TANROADS pamoja na TARURA kukutana na Taasisi au Mamlaka zilizoweka vizuizi na vituo vya ukaguzi katika maeneo hatarishi ili kuviondoa na kwa pamoja kukubaliana maeneo sahihi ya kuweka vituo hivyo.