Baada ya May 14 2017 michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 kuanza nchini Gabon katika uwanja wa Port Gentil, May 15 ilikuwa ni zamu ya michezo ya Kundi B kuchezwa katika uwanja wa Stade de Amitie jijini Libreville kwa michezo Kundi B kuchezwa.
Moja kati ya michezo iliyochezwa siku ya May 15 ni mchezo kati ya timu ya taifa ya Maliambao ndio Mabingwa watetezi dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania Serengeti Boys, mchezo huo wengi walikuwa wakitarajia kuona Mali akifanikiwa kuondoka na point tatu ukilinganisha lakini walijikuta game ikimalizika kwa sare tasa 0-0
Rekodi ni nyingi zilizokuwa zinambeba Mali ambaye ndio Bingwa mtetezi wa michuano ambapo alitwaa taji hilo 2015 akiwa kacheza jumla ya michezo mitano na kutofungwa katika michezo yote zaidi ya kuishia sare mchezo mmoja dhidi ya Afrika Kusini February 19 2015 ilikuwa sare ya 2-2 na kuambulia kufunga jumla ya magoli 10 na kuruhusu kufungwa magoli manne.
Baada ya michezo yote miwili kumalizika tukampata kocha wa Serengeti Boys Bakari Shime kuzungumzia kuhusiana na mchezo na kuhusu Angola.