Siku moja baada ya Kagera Sugar kuishushia kipigo Simba katika Uwanja wa Taifa, ligi kuu ya Tanzania bara maarufu kama Vodacom Premier League imeendelea tena jioni hii kwa mchezo kati ya Yanga SC vs Azam FC.
Katika mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, Azam ilikuwa ya kwanza kupata bao alilofunga na Didier Kavumbagu dakika 6, Yanga walisawazisha kupitia Amiss Tambwe (7) na kupata la pili lililofungwa na Simon Msuva (57), kabla ya John Bocco aliyeingia akitoa benchi kuisawazishia Azam dakika 65.
Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 14, sawa na Azam, wakati Mtibwa Sugar imebaki kileleni ikiwa na pointi 16, baada ya kulazimishwa sare 1-1 na Stand United jana asubuhi mchezo huo juzi ilivunjwa kutokana na mvua kubwa kunyesha.
Mbeya City imejiondoa mkiani baada ya kuichapa Ndanda FC 1-0, wakati Polisi Morogoro imeinyuka Mgambo JKT kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Kutoka Morogoro: Polisi Morogoro wameutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani kwa kuichapa Mgambo JKT kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Polisi ilipata bao kwanza dakika 22, lililofungwa na Nicolaus Kabipe kabla ya Iman Mapunda kupachika bao la pili kwa kichwa dakika 85, akiunganisha kona ya Kabipe.
Kutoka Mbeya: Deus Kaseke aliwainua mashabiki wa Mbeya City dakika pili kwa kufunga bao pekee akiunganisha kwa shuti lililomshinda kipa wa Ndanda FC, Salehe Marande na kujaa wavuni.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook