Stori ninayokusogezea leo March 28, 2018 ni kuhusu Tume ya mawasiliano nchini Uganda, UCC, imevifungia zaidi ya vituo 20 vya redio. Vituo hivyo vinatuhumiwa kutangaza ‘uganga wa kienyeji na kuwatapeli wananchi.’
Hatua hii inafuatia baada ya kutolewa onyo kuwa vituo hivyo viache kufanya vipindi na waganga wa kienyeji. Tangazo hilo la kufungiwa vituo vya redio 23 limetolewa jana jioni na mwenyekiti wa Tume ya Mawasiliano Godfrey Mutabazi.
Mutabazi ameshutumu redio hizo kutumiwa na waganga wa kienyeji kuwatapeli wananchi na kuvunja sheria ya uchawi ya kifungu cha pili.
Redio hizo zimekuwa zikiwapa vipindi waganga hao wa kienyeji kutangaza uganga wao, huku wakiwaambia wananchi kutuma fedha kupitia njia ya simu za mikononi.