Alhamisi ya June 29 2017 Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF Jamal Malinzi pamoja na wengine wawili akiwemo Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine walifikishwa Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kusomewa mashitaka yao.
Malinzi pamoja na wenzake walisomewa mashitaka 28 kati ya hayo 25 yanamuhusu yeye likiwemo la kutuhumiwa kutakatisha fedha, kwa mujibu wa sheria wanasema halina dhamana, baada ya hakimu Wilbroad Mashauri kuahirisha kesi hadi July 3.
Wakili msomi ambaye yupo katika jopo la mawakili wanaomtetea Jamal Malinzi na wenzake aliongea na waandishi wa habari:>>>” Tunachoiomba mahakama izingatie hoja za upande wa utetezi kama ambavyo tumezitoa kwa sababu ni hoja za kuzingatia haki.” – Komba.
VIDEO: All Goals Taifa Stars vs Lesotho June 10 2017, Full Time 1-1