Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress (ANC) kimeshindwa katika jitihada za kisheria kukizuia chama kipya kilichoundwa, kinachoungwa mkono na aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma, kushiriki katika uchaguzi mkuu wa Mei.
Chama cha uMkhonto we Sizwe (MK) kinachukua jina lake kutoka kwa mrengo uliosambaratishwa wa ANC.
Inafikiriwa kuwa uungwaji mkono wa Bw Zuma kwa MK unaweza kuathiri uungwaji mkono wa ANC.
Mahakama ya uchaguzi ilikataa hoja ya ANC kwamba chama hicho hakijatimiza vigezo rasmi vya usajili.
Wafuasi wa MK, waliovalia mavazi ya kijani, walicheza kwa furaha nje ya mahakama baada ya uamuzi huo kusomwa.
ANC imesema inakubali uamuzi huo na itauzingatia.
Katika taarifa iliyoandikwa, msemaji alisema kuwa hii haikuwa kuhusu ANC kufuatilia kesi dhidi ya MK.
Chama, aliongeza, hakipingani na uwepo wa MK kwenye kura, mradi uandikishaji uliofanywa na tume ya uchaguzi ulikuwa kwa mujibu wa sheria.
ANC pia imeanzisha kesi tofauti za kisheria dhidi ya chama cha MK, kikishutumu kwa ukiukaji wa hakimiliki.