Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) imefanya uteuzi wa makatibu wakuu wa idara makao makuu na wajumbe wa halmashauri kuu ikiwa ni maazimio ya kikao cha baraza kuu la umoja huo lililokutana Mei 23, 2021 jijini Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Mei 24, 2021 katibu mkuu wa UVCCM, Raymond Mwangwala amesema kwa mujibu wa kanuni ya umoja huo toleo la mwaka 2019 kanuni ya 87(3) ukurasa 79 baraza hilo limethibitisha uteuzi wa wakuu wa Idara za UVCCM makao makuu.
Amesema Lusekelo Mwandemange amekuwa katibu wa baraza kuu la UVCCM wa uwezeshaji, uchumi na fedha na Bilal Hussein Maulid amekuwa katibu wa baraza kuu la UVCCM wa oganaizesheni na siasa, Dollar Kusenge katibu wa baraza kuu la UVCCM wa uhusiano wa kimataifa na vyuo vikuu
Victoria Mwanziva amethibitishwa kuwa katibu wa baraza kuu la UVCCM, uhamasishaji na chipukizi.
Aidha Baraza hilo limeunda kamati ndogo ya uwezeshaji, uchumi na fedha na kuwathibitisha Fred Ngajiro maarufu Vunjabei kuwa mwenyekiti wa kamati, Rose Manumba kuwa katibu wa kamati.
Wajumbe ni Gwanta Alex, Taufiq Turky, Khamis Tale Tale maarufu Babu Tale na Khadija Ali
Baraza hilo lilifanya uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi zilizo wazi za wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM pamoja na wajumbe wa kamati ya utekelezaji ya baraza juu la UVCCM ambapo, Khadija Ismail amekuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM-Bara, Nabir Ahmed Abdallah kuwa mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM- Zanzibar na Raymond Muhenga kuwa mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya baraza kuu la UVCCM.
Pia Hussein Ayoub amechaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya baraza kuu la UVCCM na kupokea majina yaliyochaguliwa ya wajumbe wa baraza hilo kupitia wabunge wa kundi la vijana ambao ni Ngw’asi Damas Kamani, Asia Halamg, Judith Kapinga, Latifa Juakali, Munira Mustafa na wawakilishi wa viti maalum kupitia kundi la vijana ambao Hudhaima Tahir na Salha Mwinjuma.