Tunayo story kutokea kwa Askari H.105 PC Mahmoud Uzia Mohammed aliyemuokoa Chief Technician Augustine Cherehani (52) akiwa hai ndani ya Kivuko cha Mv.Nyerere kwa siku tatu kilichopinduka September 20, 2018 kutunukiwa Cheo cha kuwa Coplo.
Askari huyo amevishwa cheo hicho na Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Wana Maji, Evance Mwijage ambapo amesema Jeshi la Polisi limeundwa kisheria na linaongozwa na sheria.
Kamanda Mwijage amesema Askari huyo alijitoa mhanga ambapo alivua mtungi wa uzamiaji kwa sababu eneo la kupita lilikuwa finyu ambapo akafuatiolia ndani ya kivuko kwa kutumia tochi na kufanikiwa kumuokoa Cherehani.