Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limethibitisha kuwa miili miwili ya watoto iliyokutwa jana kwenye shimo ikiwa imeharibika katika Kata ya Olasiti ni miongoni mwa watoto waliotekwa tangu August 21, 2017.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amesema kuwa mtu aliyehusika na utekaji wa watoto anayeshikiliwa na Jeshi hilo baada ya kukamatwa mkoani Geita alieleza jana mchana baada ya uchunguzi akikiri kuhusika kuwateka watoto hao na kuwauwa kisha kuwatumbukiza katika shimo la maji machafu.
Miili ya watoto hao imetambulika kuwa ni Iqram Salum na Maurine David Ernest.
>>>”Alihusika kuwateka hawa watoto na alishawadhuru. Tuliongozana naye mpaka Olasite na kuonesha sehemu ambayo alikuwa amewaua hawa watoto na kuwatumbukiza kwenye shimo la maji machafu katika nyumba iliyojengwa hivi karibuni.”
Aidha, Kamanda Mkumbo amesema wanaendelea kumshikilia mtuhumiwa huyo na upelelezi utakapokamilika atafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
“Tunaendelea na uchunguzi na tukimalisha tutamfikisha Mahakamani.” – Kamanda Mkumbo.
UTEKAJI MWANZA: Mama asimulia kila kitu Mtoto kutekwa, Mtekaji ataka atumiwe MILIONI 3 M-Pesa
GUMZO LA UTEKAJI! Mzazi mwingine asimulia mtoto kutekwa, adaiwa MILIONI 4.5