Vyama vinane vya kisiasa nchini Kenya vimetishia kuachana na muungano mpya ulioundwa wa Azimio la Umoja-One Kenya ambao unaunga mkono mbio za urais za kiongozi wa ODM Raila Odinga.
Katika taarifa ya Jumatano, Aprili 6, vyama vilivyotambuliwa kwa pamoja kama Mwanzo Mpya vilikashifu kutengwa wakati wa kufanya maamuzi muhimu katika muungano huo.
Wakiongozwa na gavana wa Machakos Alfred Mutua, kikao hicho kililalamika kuwa hawakufahamishwa kabla ya kuundwa kwa Azimio la Umoja – One Kenya Alliance, wakisema walifahamu kupitia vyombo vya habari.