Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, leo February 13, 2019 akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha amemtaka Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, kurudi nchini ili kusaidia vyombo vya ulinzi na usalama katika upelelezi wa shambulio lake la kupigwa risasi.
Pamoja na hayo waziri Lugola amewaonya watu wote wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kumchafua na kumtukana Rais na kusema kwa kushirikiana na TCRA Watawakamata.