Mwanasheria Mkuu wa Nigeria amesema, watu waliowapiga risasi na kuua waandamanaji nchini humo hawajulikani na huenda watu waliofunika nyuso zao na kuvalia sare za kijeshi ndio waliohusika.
Abubakar Malami amesema, ni mapema sana kusema iwapo Polisi walihusika katika kuwapiga risasi waandamanaji waliokuwa wanalalamikia vitendo vya Polisi kutumia nguvu kupita kiasi.
Maandamano nchini Nigeria yaligeuka kuwa vurugu Oktoba 20 baada ya kuripotiwa Wanajeshi wamewapiga risasi baadhi ya waandamanaji mjini Lagos, muda mfupi baada ya kuwekwa masharti ya watu kusalia nyumbani kwa saa 24.
Wanajeshi na Polisi wanaripotiwa kuua watu 12 katika mitaa miwili ya Lagos Oktoba 20, kulingana na walioshuhudia pamoja tamko la Shirika la Amnesty International.
WANAMUZIKI WA BENDI WAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI