Waandishi wa habari nchini wametakiwa kutumia mdahalo wa Kitaifa kuhusu ulinzi na Usalama kwa waandishi wa habari kukumbushana miiko ya uandishi wa habari ili kuandika habari kizalendo na kwa maslahi ya taifa.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Naibu Kamishna wa Polisi(DCP) David Misime wakati akifungua mdahalo huo Machi 28, 2024 Dodoma Hotel, Jijini Dodoma uliaondaliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).
Mdahalo huo umehusisha wadau mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Klabu za Waandishi wa habari, Waandishi wa habari, Maafisa habari wa Jeshi la Polisi, Polisi Kata, Viongozi wa dini, TAMWA na MCT.