Katika kuunga Mkono Juhudi za Serikali za Kuwasaidia wananchi Wa Hanang Waliokumbwa na Mafuriko, Taasisi Mbalimbali pamoja na Makampuni ikiwemo Kampuni ya Mega Beverages Limited wazalishaji wa K-Vant na Asilia Vodka wametembelea waathirika wa mafuriko ya Hanang, mkoani Manyara na kutoa misaada ya kiutu.
“Tunaungana na watanzania wenzetu walioathirika na mafuriko ya Hanang, pia tukitekeleza wito wa Mheshimiwa Raisi Dkt. Samia Suluhu Hassan” John Obote-Meneja Ukuaji na Uendelezaji Biashara Kutoka Mega Beverages Limited
Kampuni hiyo imefanikiwa kuleta mahitaji mbalimbali kama magodoro, blankenti, Sabuni na vyakula kama maharagwe, mchele na sukari, jambo ambalo wanasema litaongeza faraja na kuwapa tumaini waathirika hao wa Mafuriko, alisema Mkami Kihwelo- Maneja utafiti na ubunifu Mega Beverages Limited
Msaada huo umepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Hanang Janeth Mayanja, kwa niaba ya Ofisi ya Waziri mkuu na kueleza kuwa Msaada huo utafikia Walengwa uku akiwaomba wadau kuongeza nguvu ya misaada kwa kuwa mahitaji bado yapo.