Jeshi la Polisi nchini Kenya, limewaachia Wabunge 11 lililowakatama kwa ajili ya mahojiano katika Kiwanja cha Ndege cha Jomo Kenyatta (JKIA), kwa tuhuma za kuwa walienda kufanya mkutano na idara ya ujasusi nchini Somalia bila idhini ya Serikali na kwamba uchunguzi zaidi unaendelea.
Wabunge hao ambao Sita ni kutoka Mandera, watatu kutoka Wajir na wawili kutoka Garisa ni Ahmed Kolosh, Ibrahim Abdi, Rashid Kassim, Mohamed Hire, Omar Maalim, Bashir Abdullahi, Adan Haji, Kullow Maalim, Adan Ali sheikh, Mohamed Dahir pamoja na Ahmed Bashane.
Kwa mujibu wa taarifa zinadai kuwa Maafisa wa Polisi, katika mahojiano na wabunge hao,walitaka kujua agenda ya mkutano huo walioufanya Somalia, ikizingatiwa kuwa Kenya na Somalia hazijakuwa na uhusiano mwema katika miaka ya hivi karibuni.
JAMAA NA DEGREE YAKE ANAPIGA DEBE STAND “NATAKA NIBADILISHE MITAZAMO YA WATU”