Wabunge 19 wa Viti Maalumu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), asubuhi hii wamefika na kuendelea na kikao cha Bunge kilichoanza leo Jumanne, Februari 2, 2021 Jijini Dodoma.
Wabunge hao wakiongozwa na Halima Mdee wameingia mjengoni wakiwa wamevalia mavazi meusi huku Mdee akiwa amevaa barakoa kwa lengo la kujikinga na maambukizo ya virusi vya corona.
Itakumbukwa Wabunge hao tayari walishavuliwa uanachama na chama chao mwishoni mwa mwaka jana kwa madai ya kukiuka utaratibu wa chama chao.