Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda amewaonya wabunge wa CCM mkoa Kigoma wasiofanya mikutano na kukutana na wananchi ili kusikiliza kero zao na kushindwa kutekeleza mipango ya maendeleo kwenye majimbo yao majina yao hatarudishwa kwenye kura za maoni kwa ajili ya kugombea tena kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Chatanda ametoa kauli hiyo kwenye mkutano wa majumuisho wa ziara yake ya siku saba mkoani Kigoma ambapo alipata nafasi ya kuzunguka kwenye majimbo manane ya mkoa huo ambapo allitembelea miradi 98 na kufanya mikutano 90 kati ya hiyo mikutano 74 ikiwa mikutano ya hadhara na wananchi.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa ipo kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya CCM chini ya Raisi Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza miradi mkoani Kigoma ambayo imeufanya mkoa huo kupiga hatua kubwa za maendeleo kuelekea kutelelea mpango wa kuufanya mkoa huo kuwa kitovu cha biashara na uchumi.
Alisema kuwa kati miradi hiyo ipo miradi ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa barabara za kiwango cha lami, mradi wa kupeleka umeme wa gridi ya Taifa,uimarishaji wa usafiri katika ziwa Tanganyika, upanuzi wa kiwanja cha ndege, miradi ya maji, afya, na elimu ambayo imekuwa chachu kuongeza shughuli za kiuchumi mkoani humo.
Mwenyekiti huyo wa UWT Taifa alisema kuwa kutekelezwa kwa miradi hiyo kuna mchango mkubwa wa ofisi ya Mkuu wa mkoa,Wakuu wa wilaya, Hlmashauri na wabunge wa mkoa huo hivyo akapongeza viongozi hao kwa kazi kubwa ya kutetea, kusimamia na kuelekeza ili mikradi itekelezwe kwa ufanisi.
Pamoja na hilo alisema kuwa apolikuwa kwenye majimbo ya mkoa huo ameona baadhi ya wabunge wamefanya kazi kubwa ya kusukuma maendeleo kwenye majimbo yao lakini baadhi ya majimbo wabunge wake wamelalamikiwa kwa kutofanya kazi na kutokuwepo kwenye majimbo yoa kwa muda mrefu.
“Wabunge wanayo maelekezo kutoka kwenye chama kuhusu kufanya mikutano, kusikiliza kero za wananchi na kuibua na kutekeleza miradi ya wananchi ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM, wanaofanya vizuri wanapongezwa lakini wasiofanya kazi majibu watayapa wakati wa mchujo wa kura za maoni, hatuwatishi muda wao wajirekebishe walipofanya hivyo panga linawahusu,”Alisema Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa UWT Taifa amewaonya watendaji wa chama hicho kwenye ngazi za mikoa, wilaya na kata kuacha kuwa wapambe wa wagombea kwa kuwakumbatiaa na kutembea nao wakati huu ambao taratibu za uchaguzi kwa ajili ya kupata wagombea wa nafasi mbalimbali haujaanza.
Akizungumza katika mkutano huo Naibu Waziri wa TAMISEMI,Zainab Katimba ameipongeza UWT kwa kufanya ziara ambazo zimeenda sambamba na ukaguzi wa miradi na kufanya mikutano hadi kwenye ngazi za vijiji ambapo mikutano hiyo ya kusikiliz kero za wananchi zimeanza kuzaa matunda.
Katimba ambaye aliongozana na Mwenyekiti huyo wa UWT kwenye majimbo yote ya mkoa Kigoma alisema kuwa wakiwa Kijiji cha Ilagala walipata kero ya tatizo la maji kwenye Kijiji hicho na mwenyekiti huyo alimpigia Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ambapo kabla hawa sasa kabla hawajamaliza ziara changamoto hiyo imeshaanza kufanyiwa kazi.