Katibu Mkuu wa Chama cha mapinduzi Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi akizungumza na Wananchi wa Maswa Mashariki amesema kuna Wabunge wanafanya kazi nzuri sana kwenye kuzungumzia shida na kero za wananchi wake wanahakikisha wanazifikisha kwenye maeneo husika hawao Chama kinawapongeza na kinawaunga Mkono lakini wale wasiosaidia Wananchi wanakushughulika na shida 2025 tutawapunguza kidogo kidogo.
“Nawaunga mkono wabunge wanaopambana kwa ajili ya maslahi ya wananchi na kuleta mabadiliko chanya. Ni muhimu kwao kuwakilisha sauti za watu wao na kusimama kidete dhidi ya vikwazo vyovyote vinavyoweza kuathiri maendeleo watu hao Chama kipo nao”
Wabunge wasiokuwa na uhusiano mzuri na wananchi mara nyingi huonekana wakikosa uelewa wa mahitaji na changamoto za jamii. Hii inaweza kuathiri maendeleo ya maeneo yao na kupelekea kutokuwapo kwa uwajibikaji na sisi Chama wakati ukifika tutawapunguza kidogo kidogo”
Katibu Mkuu Balozi Nchimbi yupo Ziara Mkoa wa simiyu akiwa anamalizia leo na atarajiwa Kesho kuanza ziara Mkoa wa Shinyanga huku akiambatana na Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu Amos Makalla pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa kimataifa Ndugu Rabia Abdalla Hamid.