Watumishi wa Bunge na Wabunge wanaoshabikia klabu za Simba na Yanga wanatarajia kuchuana katika bonanza maalumu linalotarajiwa kufanyika Februari 1, 2025 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati ya michezo ya Bunge, Festo Sanga akizungumza na waandishi wa habari ameeleza kuwa maandalizi ya bonanza hilo yamekamilika na kudhaminiwa na Benki ya Azania, litajumuisha michezo ya mpira wa miguu, pete, wavu na michezo mingine mbalimbali.
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa TFF, Waris Karia ambapo malengo makuu ya kufanyika kwa bonanza hilo ni kuongeza mahusiano baina ya bunge na taasisi nyingine za kiserikali na binafsi pamoja na kuunga mkono juhudi za Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kukuza michezo nchini.