Wabunge watatu wa upinzani nchini Uganda wanazuiliwa kizuizini tangu siku ya Jumatatu kabla ya kesi yao kusikizwa, polisi imetangaza Jumatatu usiku Julai 22.
Wabunge hao walikamatwa katika mkesha wa maandamano dhidi ya ufisadi yaliyopigwa marufuku na mamlaka.
Wanajeshi na polisi walikuwa wamegeuza ofisi za Jukwaa la Umoja wa Kitaifa (NUP) kuwa “kambi ya kijeshi”, na “wamewakamata kwa nguvu” baadhi ya maafisa wa chama, alisema.
Polisi hawakuthibitisha kukamatwa kwa watu hao, lakini inasemekana walisema kwamba walikuwa wamechukua “hatua za tahadhari” kuzuia “uhamasishaji wa maandamano”.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni alionya Jumamosi kwamba waandaji wa maandamano yaliyopangwa kwenda bungeni “wanacheza na moto”.
Vijana wa Uganda wamekuwa wakihamasisha uungwaji mkono mtandaoni kwa maandamano hayo kutaka kukomesha kile wanachosema ni viwango vya juu vya ufisadi na utawala mbaya.
Kwa kiasi fulani wamehamasishwa na wenzao katika nchi jirani ya Kenya, ambao maandamano yao ya hivi majuzi yalimlazimu rais wao kughairi mipango ya kuongeza ushuru.
Bobi Wine, nyota wa zamani wa muziki ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, alikanusha kuwa NUP ilikuwa ikiandaa maandamano nchini Uganda.
Hata hivyo, alisema chama chake kinaunga mkono “kila jitihada za kupinga dhuluma, ufisadi na utawala mbovu”.