Wabunifu wa maudhui nchini Kenya watapata pesa kwa kuchapisha kwenye mitandao ya Facebook na Instagram kuanzia Juni mwaka huu kufuatia makubaliano kati ya rais William Ruto na kiongozi wa Meta Nick Clegg.
Katika mkutano kwenye Ikulu ya Nairobi, idara ya rais mawasiliano ya rais makubaliana hayo ni kilele cha jitihada za mwaka mzima za serikali kuwa na wabunifu wa kupata mapato kutokana na maudhui yao ya mtandaoni kama wanavyofanya kwenye majukwaa mengine kama vile Youtube na X(Twitter)
“Watayarishi wa maudhui wa Kenya wanaokidhi vigezo vya kustahiki sasa watapata mapato kutokana na nafasi zao za facebook na Instagram tunapoanza uchumaji wa mapato kufikia Juni mwaka huu”, alisema Bw. Clegg.
Rais william Ruto alipongeza hatua hiyo, akibainisha kuwa itafungua fursa mpya za kuwaingizia kipato vijana wa Kenya, huku akitoa wito kwa meta kuunganisha malipo kwa M-pesa.
“Sasa waundaji wa maudhui wanaweza kuanza kuchuma mapato kutokana na mawazo na ubunifu wao. Tunatumia nafasi ya kidijitali kuunda nafasi za kazi kwa mamilioni ya vijana wasio na kazi katika nchi yetu”, Ruto alisema.