Wacheza soka nchini Italia watapigwa marufuku kuvaa jezi nambari 88 kwenye jezi zao kama sehemu ya mpango wa kupambana na chuki iliyotangazwa Jumanne.
Nambari ya 88 ni code nambari ya “Heil Hitler.”
Mnamo Machi, shabiki aliyevaa shati la Lazio lenye jina “Hitlerson” na nambari 88 juu yake alipigwa marufuku maisha kuhudhuria mechi za kilabu ya Kirumi.
Mpango huo ambao unaratibiwa kati ya serikali ya Italia na shirikisho la soka la Italia, unajumuisha kuongezwa kwa kanuni za maadili kwa mujibu wa Muungano wa Kimataifa wa Kukumbuka Mauaji ya Wayahudi.
Mpango huo pia unatoa wito kwa michezo kusimamishwa iwapo kuna nyimbo au vitendo vya chuki dhidi ya Wayahudi – sawa na jinsi kesi za ubaguzi wa rangi zinavyopaswa kushughulikiwa.