Wachezaji wa club ya Atletico Madrid ya Hispania wamekubali kila mmoja kukatwa asilimia 70 ya mshahara wake wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona ili club yao iweze kuwalipa wafanyakazi 430 wa club kama kawaida.
Wachezaji wa Atletico Madrid wanawakuwa wa pili au timu ya pili Hispania kukubali makato ya asilimia 70 ya mshahara baada ya club ya FC Barcelona kufanya hivyo na wachezaji kuridhia.
Baada ya kusimama kwa Ligi Mbalimbali za soka Ulaya, vilabu vingi vimeyumba kiuchumi kutokana na kushindwa kuzalisha, huku Juventus wao wakidaiwa kuwa mbioni kumuuliza staa wao Cristiano Ronaldo siku za usoni wakitazamia kushindwa kumlipa mshahara wa pound 500,000 kwa wiki sababu ya kiuchumi.