Wachimba migodi wote kumi na watano waliokuwa wamenaswa katika mgodi wa dhahabu wa Zimbabwe kwa siku nne wameokolewa.
Waziri wa Madini Soda Zhemu alisema wafanyakazi walikuwa na afya njema na fahamu.
Mgodi wa dhahabu wa Redwing unaomilikiwa na Metallon Corporation uliporomoka siku ya Alhamisi.
Maafisa walisema tetemeko la ardhi huenda lilisababisha ajali hiyo.
Familia za wafanyakazi waliokwama wamekuwa wakipiga kambi katika eneo la mgodi katika kijiji cha uchimbaji madini cha Penhalongato – kilomita 270 (maili 167) mashariki mwa mji mkuu Harare – wakisubiri uokoaji.
Eneo hilo ni nyumbani kwa wafanyikazi wengi wasio na hati ambao hutafuta riziki huku kukiwa na hali ngumu ya kiuchumi.