Kampuni ya Teknolojia ya Kuaishou Nchini China imeshambuliwa mtandaoni ikidaiwa kuingilia faragha na uhuru wa Wafanyakazi wake baada ya kuweka vifaa maalum vinavyohesabu muda ambao Mfanyakazi anautumia akiwa chooni. (timer)
Baada ya kuona habari yao imesambaa na kukosolewa kumezidi, Kampuni hiyo imejitetea kuwa ilifanya hivyo ili kuongeza kasi ya uzalishaji na kupunguza uzembe wa Watu kutumia muda mwingi kuperuzi mtandaoni wanapoingia vyooni Wanawake kwa Wanaume.
Nanukuu kauli ya Uongozi wa Kuaishou ikisema “Unakuta Mtu anatumia muda mwingi chooni kuliko muda anaotumia kufanya kazi, Wanawake wanaongoza kila muda chooni kuweka make up na nywele zao, anayezidisha muda tulioweka atakatwa mshahara”
Kwa miaka mingi Maboss wengi wamekua wakijaribu kuja na mbinu za kuwabana Wafanyakazi na kuhakikisha kazi zinafanyika kwa ufasaha lakini hii mpya ya China ndio toleo la kwanza la aina yake Mimi kuwahi kukutana nalo.