Uchumi wa dunia watabiriwa kukua taratibu 2024 sababu hii ni kutoimarika kwa mambo kutokana na janga la COVID-19 kimataifa, majanga ya hali ya hewa na mivutano ya kikanda inayodhoofisha zaidi maendeleo.
Ripoti Umoja wa Mataifa ya hali ya uchumi na matarajio ya 2024 ya Alhamisi, inaonyesha ukuaji wa uchumi duniani utapungua tofauti na ilivyokadiriwa mwaka 2023, kwa kati ya asilimia 2.7 na 2.4, ikiwa ni chini ya kiwango cha ukuaji kabla ya janga cha asilimia 3.
“Ukuaji mzuri uliotarajiwa 2023 ulisukumwa na mataifa kadhaa makubwa kiuchumi kama Marekani, Brazil, India na Mexico,” amesema Shantanu Mukherjee, mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi wa Uchumi na Sera katika Idara ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa.
Lakini, pia amesema ukuaji huo unaweza kupungua mwaka huu haswa kwa Marekani kwa sababu ya viwango vya juu vya riba, kupungua kwa wanunuzi na soko dhaifu la ajira.