Wataalamu wa saikososholojia wamegundua kwamba katika ulimwengu wa sasa, Chuki ni gonjwa la kuambukiza na lenye sumu hatari sana na linaloenea kwa kasi sana na kuuwa zaidi ya magonjwa mengine mengi,hivi sasa walimwengu wanahitaji kutambua na kufanya kila njia kuepuka chuki kwa ajili ya usalama wa kiafya, kiuchumi, kifamilia, kitaifa na kimataifa.
Kwa kuwa chuki ni janga na inamuathiri kila mtu, wadau mbalimbali wa maendeleo wanaalikwa katika kushiriki katika harambee ya kuwezesha Misheni ya kukabiliana na Chuki Ulimwenguni itakayofanyika mlimani city lengo ikiwa ni kuchangia pesa kwa namna watakavyoguswa. Taarifa zaidi za misheni hii zitatolewa siku ya kilele cha Harambee hii tarehe 31Julai 2024.
Katika “dinner” hiyo, wadau mbalimbali wa maendeleo wataungana katika kuwezesha na kuanzisha mipango mbalimbali ya kukabiliana na ugonjwa huu hatari wa chuki. Moja kati ya mipango hiyo ni kuwezesha Uzinduzi wa Misheni ya Kukabiliana na Chuki Ulimwenguni.
Katika kuwezesha misheni hii kutakuwa na harambee ya kutafuta fedha takribani shilingi Bilioni 2.
Matarajio baada ya “Dinner” ya Kukabiliana na Chuki:
1. Mijadala kuhusu madhara ya chuki kuibuliwa na kuenezwa kwa jamii
2. Programu kuhusu madhara ya chuki kuanzishwa na kuenezwa
3.Madhara yatokanayo na janga la Chuki kupungua mfano: ujinga, ukatili, fitina, dharau, huzuni
Jamii yetu ya Tanzania kama zilivyo jamii zote ulimwenguni inakabiliwa na ugonjwa hatari wa chuki na hivyo kusababisha maasi mengi kuongezeka na utu kupotea.
Kwa mkutadha huo A sasi ya Family Vibes Foundation kwa kushirikiana na Wadau wa nchi za falme za kiarabu wakaona umuhimu wa kuwa na Misheni ya Kukabiliana na Chuki Ulimwenguni (Universal Mission to Combat Hatred).
Uzinduzi yanayotarajiwa kufanyika Abu Dhabi, katika Falme za Kiarabu.