Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa amewataka wadau na mamlaka za Serikali kushirikiana kimamilifu ili kuzua uharibifu wa Mazingira unaotokana na Uchimbaji wa Madini kwenye vyanzo vya maji.
Mgandilwa ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha tatu cha Jukwaa la Wadau wa usimamizi wa rasilimali za maji cha mto zigi Mkoani hapo.
Akizungumza na wadau mbalimbali wa Sekta na watumiaji wa maji ambapo amesema kuwa ni wajibu wa mamlaka na wadau wote kwa ujumla kushiriki kikamilifu ilinda vyanzo vya maji kwa kwa wilaya ya muheza hususa milima ya amani kuna changamoto kubwa ya uchimbaji wa Madini kwenye vyanzo hivyo hivyo ni muhimu kushiriki kwa pamoja kutokomeza uharibifu huo.
“Lakini natambua bado tuna changamoto kubwa kwenye maeneo yetu ya vyanzo vya maji tuna jua mazingira ukiyaharibu leo nayo yatakuadhibu kesho hivyo tuna kila sababu kuendelea kusimamia na kudhibiti uharibifu wa mazingira kwenye vyanzo vya maji hususani uchimbaji madini ya dhahabu na mchanga kwenye maeneo hayo”-Alisema Mgandilwa.
Aidha Mgandilwa ameiomba wadau kuendelea kutoa Elimu juu ya baadhi ya Wananchi wanaofanya shughuli za kilimo kwenye vyanzo vya Maji kwani kufanya hivyo ni kupelekea adha ya ukosefu wa Maji kwenye maeneo mengine.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa bonde la maji Bonde la pangani Segule Segule amesema kuwa lengo la jukwaa hilo la wadau ni kujadili changamoto zinazotokea kwenye eneo la bonde la Pangani ambapo Mkoa wa Tanga una hudumiwa na kidakio cha mto zigi hivyo kujaa tope kwenye kidakio hicho kinapeleka adha kubwa kwa Wananchi ambao ni watumiaji wa maji kutoka mji wa Tanga pamoja na Wilaya ya Muheza.
“Kwakweli Jukwaa hili litasaidia kwa pamoja kutatua changamoto mbalimbali zinazo kabili kidakio cha mto zigi kama ukataji wa miti na kufanya kilimo kwenye vyanzo vya maji”- Alisema Segule Segule.