Wadau wa maendeleo wameendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kumkomboa mwanamke dhidi ya matumizi ya mkaa, kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya gesi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Jamii Foundation, Jackline Maloa, amesema kuwa mpango huu ni muhimu katika kuboresha maisha ya wanawake na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Ameongeza kuwa kupitia miradi ya nishati safi, wanawake watapata fursa ya kutumia muda wao kwa shughuli za kiuchumi, badala ya kutumia muda mwingi kutafuta mkaa.
Kwa upande mwingine, Mkurugenzi Mtendaji wa Caliber First Group, Sylvia Mohamed Mkomwa, ameongeza kuwa shirika lao linaendelea kujikita katika kuhakikisha wanatengeneza jamii yenye nguvu na inayojitegemea na kusisitiza kuwa wataendelea kuunga mkono juhudi hizi na kutoa mchango wao katika kuboresha maisha ya wanawake, huku wakitafuta njia bora za kukuza matumizi ya nishati safi katika jamii.