Serikali imeshauriwa kutengeneza sheria itakayoelekeza halmashauri nchini kutenga angalau asilimia moja ya mapato ya ndani kwa ajili ya afua zinazojihusisha na masuala ya jinsia na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Hayo yamebainishwa wakati wa Kongamano la wadau wa asasi za kiraia kwa kushirikiana na Halmashauri ya jiji la Tanga na ngazi ya kata la kujadili juu ya mkakati wa kuimarisha uwezo wa kitaifa wa kukabiliana na athari mbaya za mbadiliko ya tabia ya nchi na kutambua jinsia kama kipengele Muhimu.
Akizungumza na wanahabari mara baada ya kongamano hilo mkurugenzi wa Tree of Hope Fortunata Manyeresa alisema lengo la kongamano hilo ni kuangalia namna bora ya kushirikiana na jamii na serikali kwanzia kangazi ya kata kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha baadhi ya wadau wa mabadiliko ya tabia ya nchi kutoka asasi mbalimbali wamesema kuwa dhana nzima ya mabadiliko ya tabia ya nchi ni kuongeza uelewa kwa jamii juu ya mabadiliko ya taibai ya nchini.
“lengo la kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi yanaanza na muungano tukishirikiana kwa ujumla baina ya serikali na asasi za kiraia wakishirikiana kwa pamoja wanaweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi,kwani serikali ina sera na sheria dhidi ya mapambano ya mabadilo ya tabia ya nchi”
“kwaupande wake Zamoyoni Mohamed amebaye ni afisa mazingira wa jiji la Tanga alisema kuwa wao kama wadau wa mazingira kila mmoja kwa nafasi yake anatakiwa kuchukua hatua ili kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama”
Hata hivyo kwa mara ya kwanza ndani ya Mkoa wa Tanga kutafanyika mbio za marathoni maalumu za kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi kwaajili ya kuhamasisha jamii kushiriki kwa pamoja kupamba na adhari mbali za mabadiliko ya Tabia ya nchi.