Kamishina wa TRA idara ya Uchunguzi na kodi Evarist Mashiba amesema mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana pamoja na wafanyabishara nchini ili kuweka mazingira rafiki ya ulipaji kodi hasa kwa wadaiwa sugu
Mashiba amesema hayo wakati wa kilele cha wiki ya Mlipa Kodi Mkoa Morogoro ambapo amesema wanakila sababu ya kujivunia kutokana na ongezeko kubwa ya ukusanyaji wa mapato Nchini ambapo umesababishwa na mazingira rafiki kati ya pande hizo mbili
Amesema Mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa morogoro imetakiwa kuendelea kujenga mahusiano mazuri na wafanyabiashara ambao pia ndio walipa Kodi Ili waweze kulipa Kodi Kwa hiari bila shuruti.
Aidha alisema kuwapo kwa mafanikio haya kumetokana na ushirikiano mzuri kati ya TRA, viongozi wa serikali na wadau wote pamoja na kampeni za tuwajibike ambazo zimeleta mafanikio na matumizi mazuri ya mbinu waliyojiweka katika mkoa wa morogoro.
Mashiba pia ametoa wito kwa wadau na wafanyabishara wote kuendelea kutoa ushirikiano na kutimiza wajibu wao ikiwa pamoja na kujisajili na kupata namba ya mlipa Kodi ili kuiwezesha Serikali kufanya maendeleo katika jamii.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Gairo Jabir Makame alimwakilisha Mkuu wa Mkoa Morogoro Adam Malima ,Makame amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kukwepa kulipa Kodi Kwa kutoa risiti ipasavyo na hivyo kuikosesha mapato serikali ambayo unatumika Kodi Kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo.
Makame amesema elimu zaidi inahitajika kwa wafanyabishara kutambua umuhimu wa kulipa kodi ili serikali iweze kuendelea kujenga miundombinu mbalimbali .