Baada ya kuwepo kwa Vitendo vya ukatili kwa wafanyakazi wa ndani ikiwemo ,kunyimwa mishahara,kulipwa ujira mdogo,kubakwa na vipigo kutoa kwa wajiri wao Serikali inawataka wenyeviti wa mitaa kuwasajili na kuwaingiza katika kazi data ya wakazi kwenye mitaa ili waweze kutambuliwa.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo kwa wawezeshaji wa haki za jamii(CJFs) na wasaidizi wa kisheria (PSW)na wenyeviti wa mitaa Afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Morogoro Faraja Maduhu amesema Vitendo hivyo vinatokea kwa sababu kundi hilo linakua halitambuliki mtaani na kukosa sehemu ya kuelezea changamoto zao.
Anasema licha ya serikali kuendelea kutoa elimu bado baadhi ya waajiri wamekua wakiwafanyia Vitendo vya ukatili wafanyakazi wao wa ndani huku wenyewe wakishindwa kutoa malalamiko yao na viongozi kushindwa kuwajibika kuwasaidia.
Anasema kitendo cha kuwasajili katika daftari la mtaa kutasaidia kupata taarifa kamili za mfanyakazi na pindi anapofanya ukatili au kufanyiwa ni rahisi kwa viongozi wa maeneo husika kuchukua hatua za kisheria .
Anaongeza kwa kusema licha ya wafanyakazi kulalamika kufanyiwa ukatili na waajiri lakini pia nao wamekua wakifanya ukatili hasa kwa watoto wa wajiri wao na kukimbia hivyo utambuzi kwenye mitaa kutasaidia kudthibiti janga hilo
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la CVM Maria Chimba ambao ndio wafadhili wa mafunzo hayo amesema lengo la kuwakutanisha ni kujadili masuala mbalimbali ili waweze kuwaelimisha wafanyakazi kutambua haki zao za kimsingi ikiwemo likizo na mikataba ya maandishi.
Anasema viongozi wa mitaa ndio msingi mkuu katika kuwasadia wafanyakazi wa ndani ni rahisi kuwafikia na kuwapa elimu ili waweze kutambua iwasaidie.
Maria ameongeza Kuwa shirika linatarajia kusaidia wafanyakazi wa ndani kwenye mikoa nane Nchini kupata mafunzo ya ufundi standi VETA kupata ujuzi wa fani mbalimbali.
Nao wenyeviti wa mitaa wamemshukuru Elimu waliyopata na kuahidi kuifikisha kwa wananchi watambue mfanyakazi wa ndani na haki kama wafanyakazi wengine huku wakisema baada ya kupatiwa elimu hiyo Vitendo vya ukatili vitapungua.