Wizara ya elimu ya Ethiopia imetangaza kufungwa kwa muda kwa shule zote za sekondari ili kuruhusu wanafunzi kusaidia katika kuvuna mazao ya Waethiopia walio kwenye mstari wa mbele vitani, Shirika la Utangazaji la Fana (FBC) linaripoti.
Waziri wa Elimu Berhanu Nega alisema shule hizo zitafungwa kwa wiki moja.
Siku ya Jumatatu, serikali ilisema zaidi ya wanafunzi milioni 1.2 hawakuwa shuleni kutokana na mzozo unaoendelea kaskazini mwa nchi hiyo, mapigano hayo pia yameharibu mamia ya shule.
Serikali ilitangaza hali ya hatari ya miezi sita mnamo Novemba ili kuzuia hatua za waasi wa Tigray kuelekea mji mkuu, Addis Ababa.