Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, amesema Wagombea wa CHADEMA ambao walienguliwa kwa mizengwe na Wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa upande wa Uenyekiti wa Kijiji ni 6,263 kati ya 10,438 ambao ni sawa na 60%.
Akiongea Jijini Dar es salaam leo December 10,2024, Mbowe amesema “Baada ya sarakasi zote za kufunga ofisi, kunyima Wagombea fomu, kuwaengua kwa mizengwe na kuacha kuwateua Chama kilibaki na Wagombea wafuatao, Wagombea wa Uenyekiti wa Mtaa walikuwa 2,686 (63%), Wagombea wa Uenyekiti wa Vijiji walikuwa 4,175 (34%) na Wagombea wa Uenyekiti wa Kitongoji walikuwa 19,805 (31%) ambapo idadi ya jumla ya Wagombea wote wa nafasi za Uenyekiti walikuwa 26,666 (33.2%)”
“Wagombea wa Chadema ambao walienguliwa kwa mizengwe na Wasimamizi wa Uchaguzi ni kama ifuatavyo, Uenyekiti wa Mtaa 1,152 kati ya 3,838 (30%), Uenyekiti wa Kijiji ni 6,263 kati ya 10,438 (60%)
“Uenyekiti wa Kitongoji ni 28,110 kati ya 47,915 (59%) ambapo Jumla ni 35,525 kati ya 62,191 (57%)”