Wizara ya Afya Zanzibar imesema kuna ongezeko la wagonjwa 6 wa corona na kufanya idadi ya wagonjwa Zanzibar kufikia 24, wagonjwa wote ni Raia wa Tanzania, Wanaume 5 na Mwanamke mmoja,hawana historia ya kusafiri nje ya Nchi siku za karibuni,kwa idadi hii sasa Tanzania ina visa 94.